Saturday, May 21, 2011

KUSAIDIA USAFIRI KWA WANFUNZI WA SHULE MANISPAA YA MTWARA-MIKINDANI

Hali ya usafiri kwa wanafunzi wa Manispaa ya Mtwara – Mikindani hasa wale wanaosoma katika shule zilizoko pembezoni mwa Manispaa ilikuwa ni ngumu sana kutokana na kutokuwa na usafiri wa uhakika, hali iliyokuwa inawafanya wanafunzi hao kupanda malori ya mchanga ili kufikia shule zao au kurudi nyumbani.  Hali hii ilichangia kwa kiasi fulani kushuka kwa kiwango cha elimu kwa wanafunzi hao na kupelekea kuwa na matokeo mabaya katika mitihani yao.
Msaada:
Katika kukabiliana na hilo, Mheshimiwa Mbunge ameweza kutoa mabasi mawili ya wanafunzi ili kuwa na usafiri wa uhakika wa kuwahudumia wanafunzi hawa.  Hali hii imeboresha kwa kiasi kikubwa hali ya usafiri wa wanafunzi wanaosoma katika shule za sekondari za Naliendele, Mangamba na Mikindani.

MBUNGE ATOA MABASI KUBEBA WANAFUNZI BURE.. GAZETI LA MWANANCHI TAREHE 21-3-2011

TATIZO la kuchelewa shuleni kwa wanafunzi wa shule za sekondari wanaosoma Kando ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani, limefika mwisho baada ya mbunge wa jimbo hilo, Hasnein Murji kutoa mabasi mawili kwa ajili ya kusafirisha wanafunzi hao.
Mabasi hayo yatasafirisha wanafunzi bure kwa lengo la kuwawezesha kuwahi kwenda na kurudi shuleni hali itakayoongeza ushiriki wa wanafunzi katika masomo hivyo kukuza taaluma shuleni.
Akizungumza na Mwananchi jana mjini Mtwara, mbunge huyo  alisema kati ya mabasi hayo, moja litasafirisha wanafunzi kutoka kituo kikuu cha mabasi hadi Naliendele umbali wa zaidi ya kilomita 10, ambalo litabeba wanafunzi wanaosoma shule za sekondari za maeneo hayo.
Alifafanua kuwa basi lingine litaanza safari zake kituo kikuu cha mabasi cha mjini hapa na kuelekea Mikindani umbali wa zaidi ya kilomita nane na kwamba msaada huo pia unalenga kumpunguzia mzazi gharama za kusomesha.
“Nimetoa mabasi mawili kwa ajili ya kusafirisha wanafunzi, basi linalokwenda Naliendele tayari limeanza safari, wakati gari la Mikindani linataraji kuanza kutoa huduma hiyo mwishoni mwa wiki hii, huu ni utekelezaji wa ahadi yangu niliyoitoa wakati wa kampeni” alisema Murji
Aliongeza kuwa “Ni imani yangu kuwa wazazi hawataniangusha, pesa waliyokuwa wanaitumia kwa ajili ya nauli sasa waitumie kwa kuwatimizia mahitaji mengine ya shule watoto wao ili tuweze kufikia lengo la kukuza taaluma, haya ni mabasi aina ya ‘Coaster’ ambayo awali nilikuwa nayatumia kwa ajili ya kusafirisha abiria”, alisema.
Baadhi ya wanafunzi wanaosoma Shule ya Sekondari ya Naliendele walielezea kufurahishwa kwao kwa utekelezaji wa haraka wa ahadi hiyo kwani imewaondolea adha ya kusafiri kwa baiskeli, miguu kwenda na kurudi hivyo kuathiri ushiriki wao katika masomo.
“Tulikuwa tunaingia darasani  saa tatu na wakati mwingine saa nne, wakati huo tayari walimu wanakuwa wameingia darasani, hata kwa wale wenye pesa usafiri ulikuwa wa shida sana, kwa hili tunamshukuru sana mbunge wetu” alisema Jasmini Abdallah
Kwa upande wao wananchi wa jimbo hilo pia walimpongeza Murji kwa uwamuzi wake huo ambao walisema utawanufaisha wananchi wote wa jimbo hilo na kutoa wito kuendelea na utekelezaji wa ahadi zingine.
“Mbali ya faida anayopata mzazi kwa kupunguziwa gharama za kusomesha, wasomi watakaotoka kwenye shule hizo watainufaisha Mtwara na Taifa kwa ujumla, nampongeza mbunge katika hili na kumtaka aendelee na utekelezaji wake wa ahadi zingine” alisema Issa Msuo Mwenyekiti wa Kijiji cha Mkangala Kata ya Naliendele.

KONGAMANO LA UZINDUZI WA KLABU YA WANACHUO WA SAYANSI YA JAMII,CHUO KIKUU CHA SAUTI,TAWI LA MTWARA


Wanachuo wanaosoma kozi ya Sayansi jamii wamezindua klabu ya wanachuo itakayoshughulikia mambo mbalimbali ya kijamii katika Manispaa ya Mtwara-Mikindani na vitongoji vyake. 
LENGO
Lengo kuu la kuanzisha klabu hii ni kuweza kutoa mchango wao katika kusaidia shughuli mbalimbali za kijamii katika eneo la Manispaa na vitongoji vyake.  Klabu pia inakusudia kuwa na mtandao mpana wa kimahusiano na wadau mbalimbali wa maswala ya kijamii na kimaendeleo.
MSAADA:  Klabu ya wanachuo wa sayansi jamii waliwasilisha barua ya kumualika Mheshimiwa Mbunge na pia kuomba mchango ili kufanikisha uzinduzi huo.  Mheshimiwa Mbunge aliweza kutoa mchango wake wa Tshs. 290,000/= na kuwataka radhi kwa kushindwa kuhudhuria uzinduzi huo kutokana na kuwa nje ya jimbo lake kwa shughuli za kikazi.
SHUKRANI:  Mwenyekiti wa kongamano alitumia fursa ya kufunga kongamano hilo kwa kutoa shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Murji kwa mchango wake mkubwa wa kufanikisha shughuli hiyo.  Wanachuo walishukuru kwa kupiga makofi kwani katika ripoti ya mwenyekiti ilionyesha kuwa ni Mheshimiwa Mbunge pekee ameweza kutoa mchango mkubwa ingawa wadau mbalimbali wa maendeleo waliweza alikwa na kuombwa mchango.  Msaada huo unaonyesha kuanza kuwabadilisha fikra za wanachuo hao katika swala zima la imani za kisiasa.

Friday, May 20, 2011

UJENZI WA SOKO YA KIJIJI CHA MBAE KATA YA UFOKONI ULIYOGHARIMU SHS 8,000,000/=

HALI YA AWALI LA SOKO LA KIJIJI CHA MBAE KABLA YA KUBOMOLEWA AN KUJENGWA UPYA NA MH HASNAIN MURJI
       HALI YA SOKO LA KIJIJI CHA MBAE HIVI SASA BAADA YA UJENZI KUKAMILIKA

 MWENYEKITI WA SOKO HILO MZEE DADI AKIFURAHIA BAADA YA SOKO KUKAMILIKA
  WAFANYABIASHARA WADOGO WA SOKO HILO WAFURAHIA SOKO JIPYA
WAFANYABIASHARA WAFURAHIA BAADA YA AHADI YA MBUNGE KUTEKELEZWA

    SOKO LA KIJIJI CHA MBAE
Wakazi wa kijiji cha Mbae walimuomba Mheshimiwa Mbunge wa Manispaa ya Mtwara – Mikindani kuwajengea soko bora la kijiji.  Hii imetokana na ubovu wa soko lao ambalo halikidhi hali bora ya soko, na limekuwa linavuja mvua ikinyesha kutokana na kuezekwa kwa makuti na kujengwa kwa miti kiasi cha kuhatarisha usalama wa wafanya biashara, afya na ubora wa bidhaa zao.
Jamii ya Mbae wamesifu na kushukuru sana utekelezaji wa ahadi alizozitoa Mheshimiwa Murji kwao.  Misaada inayoelekezwa kwao ina lengo la kuimarisha huduma za kijamii na kiuchumi.
Shukrani za dhati toka kwa wakazi wa Mbae:
Wakazi wa Mbae wameweza kutoa shukrani zao za dhati kwa Mbunge wao Mheshimiwa Murji kwa kutimiza kwa vitendo ahadi zake za kusaidia shughuli za kijamii ambazo zinaleta maendeleo kwao.                                            

HASNAIN MOHAMMED MURJI: UKARABATI WA HALI YA JUU MSKITI WA MBAE KATA YA UF...

HASNAIN MOHAMMED MURJI: UKARABATI WA HALI YA JUU MSKITI WA MBAE KATA YA UF...: "1. UKARABATI WA MSIKITI WA KIJIJI CHA MBAE Katika kuhudumia jamii na wanainchi kwa ujumla, Mheshimiwa Mbunge wa Manispaa ya Mtwara – ..."
  SURA YA MBELE MSKITI WA MBAE BAADA KUKAMILIKA UKARABATI WA HALI YA JU ULIOFANYIKA NA MBUNGE WA MTWARA MJINI MH HASNAIN MURJI             








VIONGOZI WA MSKITI WA MBAE KWA PAMOJA WATOA SHUKRANI ZA DHATI KWA MBUNGE WAO MH MURJI
  

UKARABATI WA HALI YA JUU MSKITI WA MBAE KATA YA UFUKONI UMEGHARIMU SH 10,000,000


1.      UKARABATI WA MSIKITI WA KIJIJI CHA MBAE
Katika kuhudumia jamii na wanainchi kwa ujumla, Mheshimiwa Mbunge wa Manispaa ya Mtwara – Mikindani ameweza kusikiliza na kutoa huduma za kijamii katika kipindi kifupi sana toka wanainchi hao wamchague kwa kura nyingi za kishindo.  Miongoni mwa shughuli za kijamii alizoanza kuzitekeleza Mheshimiwa Murji ni pamoja na kukarabati msikiti wa kijiji cha Mbae utakaowawezesha wakazi wa kijiji hicho kuwa na msikiti mzuri na wa kisasa katika kuendesha vema ibada kulingana na imani yao ya dini ya Kiislamu. Ukarabati na umaliziaji wa ujenzi msikiti wa kijiji cha Mbae umefanyika kwa kiwango kikubwa.  Ukarabati huo umehusisha msikiti wenyewe, madrasa na vyoo.                               Viongozi na waumini wafuatao waliweza kutoa shukrani zao za dhati kwa Mheshimiwa Mbunge:
·         Mr. Dadi Hamisi – Mwenyekiti wa msikiti
·         Shafii Ally Mmedi – Imamu Mkuu
·         Shaibu Dadi Hassan – Imamu Msaidizi
·         Mr. Salum Abdallah Lingondo – Mzee wa msikiti
·         Mr. Ahmad Ahmad – Mzee wa msikiti
·         Ismail Ahmad Ponda – Muumini
·         Mohamed Salum Lingondo – Muumini
·         Hassani Silim Mtondo – Muumini
·         Mr Mtiko – Msimamizi wa ujenzi na ukarabati wa msikiti.

Katika kudhibitisha ukarabati huo, wakazi na waumini wa Msikiti huo wa Mbae walishukuru kwa hatua mzuri ya ukarabati wa msikiti huo.  Pia walimshukuru Mbunge wa Manispaa ya Mtwara – Mikindani Mheshimiwa Murji kwa kutimiza ahadi alizoahidi wakazi wa kijiji hicho. 
GHARAMA ZILIZOTUMIKA KATIKA UJENZI NA UKARABARI WA MSIKITI
Jumla ya Tsh10,000,000/=. zimetumika katika ukarabati wa msikiti huo ambao umehusisha msikiti wenyewe, madrasa na vyoo.