Saturday, May 21, 2011

KONGAMANO LA UZINDUZI WA KLABU YA WANACHUO WA SAYANSI YA JAMII,CHUO KIKUU CHA SAUTI,TAWI LA MTWARA


Wanachuo wanaosoma kozi ya Sayansi jamii wamezindua klabu ya wanachuo itakayoshughulikia mambo mbalimbali ya kijamii katika Manispaa ya Mtwara-Mikindani na vitongoji vyake. 
LENGO
Lengo kuu la kuanzisha klabu hii ni kuweza kutoa mchango wao katika kusaidia shughuli mbalimbali za kijamii katika eneo la Manispaa na vitongoji vyake.  Klabu pia inakusudia kuwa na mtandao mpana wa kimahusiano na wadau mbalimbali wa maswala ya kijamii na kimaendeleo.
MSAADA:  Klabu ya wanachuo wa sayansi jamii waliwasilisha barua ya kumualika Mheshimiwa Mbunge na pia kuomba mchango ili kufanikisha uzinduzi huo.  Mheshimiwa Mbunge aliweza kutoa mchango wake wa Tshs. 290,000/= na kuwataka radhi kwa kushindwa kuhudhuria uzinduzi huo kutokana na kuwa nje ya jimbo lake kwa shughuli za kikazi.
SHUKRANI:  Mwenyekiti wa kongamano alitumia fursa ya kufunga kongamano hilo kwa kutoa shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Murji kwa mchango wake mkubwa wa kufanikisha shughuli hiyo.  Wanachuo walishukuru kwa kupiga makofi kwani katika ripoti ya mwenyekiti ilionyesha kuwa ni Mheshimiwa Mbunge pekee ameweza kutoa mchango mkubwa ingawa wadau mbalimbali wa maendeleo waliweza alikwa na kuombwa mchango.  Msaada huo unaonyesha kuanza kuwabadilisha fikra za wanachuo hao katika swala zima la imani za kisiasa.

No comments:

Post a Comment