MWENYEKITI WA SOKO HILO MZEE DADI AKIFURAHIA BAADA YA SOKO KUKAMILIKA
WAFANYABIASHARA WADOGO WA SOKO HILO WAFURAHIA SOKO JIPYA
WAFANYABIASHARA WAFURAHIA BAADA YA AHADI YA MBUNGE KUTEKELEZWA
SOKO LA KIJIJI CHA MBAE
Wakazi wa kijiji cha Mbae walimuomba Mheshimiwa Mbunge wa Manispaa ya Mtwara – Mikindani kuwajengea soko bora la kijiji. Hii imetokana na ubovu wa soko lao ambalo halikidhi hali bora ya soko, na limekuwa linavuja mvua ikinyesha kutokana na kuezekwa kwa makuti na kujengwa kwa miti kiasi cha kuhatarisha usalama wa wafanya biashara, afya na ubora wa bidhaa zao.
Shukrani za dhati toka kwa wakazi wa Mbae:
Wakazi wa Mbae wameweza kutoa shukrani zao za dhati kwa Mbunge wao Mheshimiwa Murji kwa kutimiza kwa vitendo ahadi zake za kusaidia shughuli za kijamii ambazo zinaleta maendeleo kwao.
No comments:
Post a Comment